Stuttgart,Ujerumani.
BAADA ya kushindwa kupata kibali cha kucheza soka Uingereza,Arsenal,imemtoa kwa mkopo wa msimu mmoja Mshambuliaji wake Mjapan Takuma Asano kwenda VFB Stuttgart inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Ujerumani.
Takuma,21,alijiunga na Arsenal mwezi Julai kwa dau la £5m akitokea Sanfrecce Hiroshima ya nyumbani kwao Japan lakini kutokana na kushindwa kukidhi vigezo vya kucheza soka nchini Uingereza amelazimika kujiunga na VFB Stuttgart kwa mkopo wa msimu mmoja ili kupata uzoefu wa kucheza soka Ulaya pamoja na kujiongezea sifa za kucheza ligi kuu nchini Uingereza.
0 comments:
Post a Comment