London,Uingereza.
BAADA ya ngoja ngoja nyingi hatimaye Arsenal imemtangaza Mshambuliaji Lucas Perez kuwa nyota wake mpya.
Perez,27,amejiunga na Arsenal akitokea Deportivo La Coruna kwa ada ya £17m.Amesaini miaka minne na atakuwa akipokea mshahara wa £40,000 kwa wiki.
Perez wenye uwezo wa kucheza kama mshambuliaji wa kati ama winga wa kushoto anaiacha Deportivo La Coruna akiwa ameifungia mabao 24 na kutengeneza (assists) mengine 17 katika michezo 58.
Kabla ya kutua La Coruna,Perez aliwahi kuvichezea vilabu vya Atletico Madrid C,Rayo Vallecano,Karpaty Lviv ya Ukraine pamoja na PAOK ya Ugiriki.
0 comments:
Post a Comment