Barcelona, Hispania.
BARCELONA imeongeza sura nyingine mpya katika kikosi chake hii ni baada ya mchana huu kutangaza kumsajili mlinda mlango wa Uholanzi,Jasper Cillessen,kutoka Ajax kwa ada ya €14 m.
Cillessen mwenye umri wa miaka 27 amesaini mkataba wa miaka mitano utakaomweka Barcelona mpaka mwaka 2021 na anatarajiwa kuanza kuichezea klabu hiyo Jumamosi hii pale itakaposhuka dimbani kupepetana na Athletic Bilbao akichukua nafasi ya Andre ter Stegen aliye majeruhi.
Barcelona imeamua kumsajili Cillessen ili kuwa mbadala wa Claudio Bravo anayekaribia kujiunga na Manchester City kwa dau la £17m.
Cillessen alijiunga na Ajax mwaka 2011 akitokea NEC Nijmegen na kufanikiwa kuichezea michezo 141.
Taarifa kutoka Uholanzi zinasema Ajax itaziba pengo la Cillessen kwa kumsajili mlinda mlango wa Newcastle United,Tim Krul,kwa mkopo wa msimu mmoja.
0 comments:
Post a Comment