728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, August 30, 2016

    NAHODHA CLAUDIO BRAVO AACHWA KIKOSI CHA CHILE

    Santiago,Chile.

    MLINDA Mlango mpya wa Manchester City,Claudio Bravo,ameachwa nje ya kikosi cha Chile ambacho kimeanza kambi kwa ajili ya kujiandaa na michezo ya kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya kombe la dunia la mwaka 2018 nchini Urusi.

    Taarifa iliyotolewa katika tovuti rasmi ya chama cha soka cha Chile,Asociacion Nacional de Futbol Profesional,imesema Nahodha Claudio Bravo,33,ameachwa kwa sababu binafsi na za kifamilia na nafasi yake itazibwa na Cristopher Trozelli.

    Michezo ambayo Bravo ataikosa ni ule wa Septemba 1 dhidi ya Paraguay na ule wa Septemba 6 dhidi ya Bolivia.

    Kwa sasa Chile iko nafasi ya nne katika kundi lake la D na timu nne za juu ndizo zitakazopata nafasi ya kufuzu michuano ya kombe la dunia.

    Kikosi Kamili.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: NAHODHA CLAUDIO BRAVO AACHWA KIKOSI CHA CHILE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top