728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, August 21, 2016

    TAKUMA WA ARSENAL ANYIMWA KIBARI CHA KUCHEZA SOKA UINGEREZA


    London,Uingereza.

    MAJALIWA ya Arsenal kumtumia Mshambuliaji wake Mpya Mjapan,Takuma Asano,katika michezo ya ligi kuu ya msimu huu wa 2016/17 yamegonga mwamba mgumu baada ya Mkali huyo kunyimwa kibari cha kufanyia Kazi nchini Uingereza.

    Takuma,21,aliyejiunga na Arsenal mwezi Julai kwa ada ya £5m akitokea Sanfrecce Hiroshima ya nyumbani kwao Japan alitazmiwa kuingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza cha Kocha Arsene Wenger lakini mamlaka za nchini Uingereza zinazohusika na masuala ya kazi na ajira zimemnyima kibari cha Kazi (Work Permit) Kutokana na kutokuwa na vigezo vya kucheza ligi kuu ya nchini humo.


    Ili mchezaji aweze kucheza ligi kuu Uingereza anapaswa kuwa na vigezo/sifa zifuatavyo:Awe raia wa Umoja wa Ulaya,Awe amecheza soka Ulaya,Awe ameitumikia timu yake ya taifa kwa asilimia sabini,Awe anatokea katika taifa linaloshika nafasi 70 za juu za ubora wa soka duniani na kadhalika.

    Sasa hii ina maana kwamba Arsenal italazimika kumtoa Takuma kwa mkopo kisha isajili mshambuliaji mwingine kabla ya dirisha la usajili barani Ulaya halijafungwa baadae mwezi huu.

    Hii ni tukio la pili kwa Arsenal kuwekewa ngumu kuwatumia wachezaji wake wapya katika kipindi kisichozidi miaka minne.Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2012 pale Joel Campbell aliponyimwa kibari cha kufanyia Kazi nchini Uingereza kutokana na kushindwa kufikia vigezo stahiki lakini baada ya miaka miwili ya kucheza kwa mkopo Ufaranaa na Ugiriki alipewa kibari na akaruhusiwa kuichezea Arsenal.Takuma nae atapaswa kupitia njia hii ili aweze kuichezea Arsenal.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TAKUMA WA ARSENAL ANYIMWA KIBARI CHA KUCHEZA SOKA UINGEREZA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top