London,Uingereza.
HATIMAYE Chelsea imemsajili kwa mara ya pili beki wa kimataifa wa Brazil,David Luiz,lakini safari hii akitokea Paris Saint-Germain ya Ufaransa kwa ada ya £38m (€45m).
Luiz mwenye umri wa miaka 29 sasa amerejea Chelsea ikiwa ni miaka miwili tu imepita tangu aihame klabu hiyo na kujiunga na Paris Saint-Germain kwa ada ya £50m.
Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa juu ya urefu wa mkataba aliosaini beki huyo mwenye uwezo wa kucheza pia kama kiungo wa ulinzi.
0 comments:
Post a Comment