728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, August 27, 2016

    KWA HILI LA MAVUGO NA AJIB,OMOG UKO SAHIHI


    Na.Paul Manjale.

    MAPEMA wiki hii kocha mkuu wa Simba SC,Joseph Omog,aliwakalisha kitimoto washambuliaji wake Laudit Mavugo na Ibrahim Ajib na na kuwataka kuacha ubinafsi wanapokuwa uwanjani na badala yake wacheze kwa kushirikiana.

    Binafsi nampongeza Omog kwa kulitambua hilo na kuanza kulipigia kelele mapema kabla mambo hayajaharibika kwani ziko Athari nyingi zitokanazo na wachezaji kucheza kichoyo na kibinafsi.Moja kati ya hizo ni timu kushindwa kupata matokeo makubwa  na mazuri uwanjani.

    Mavugo na Ajib wanapaswa kutambua kwamba kitakachoiletea  mafaniko Simba SC ni ushirikiano na juhudi zao uwanjani na si kitu kingine. 

    Uchoyo,ubinafsi na kutaka kuonyeshana umwamba nani anajua zaidi ya mwingine havitaisaidia Simba SC katika kipindi hiki inachohaha kurejesha makali yake ya zamani.

    Simba SC inahitaji kitu cha ziada zaidi ya uchoyo wa Mavugo na ubinafsi wa Ajib na ndiyo maana kwa kuliona hilo kocha Omog ameamua kuwakemea mchana kweupe.

    Acha niwakumbushe labda wamesahau,lengo la Simba SC msimu huu ni kutwaa ubingwa wa ligi kuu bara. Ipate nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa na hatimaye iweze kuondokana na jina la wa matopeni.

    Mavugo na Ajib wanapaswa kutambua kuwa Simba SC ina deni kubwa kwa wanachama na mashabiki wake na ushirikiano wao pamoja na ule wa wachezaji wengine ndiyo utakaolilipa.

    Wanapaswa kujifunza kutoka kwa Amiss Tambwe na Donald Ngoma ambao ushirikiano wao kwa kiasi kikubwa ndiyo ulioipa Yanga SC taji la ligi kuu msimu uliopita.

    Iko mifano mingi ya wachezaji walioshindwa kuzibeba timu zao kwa kuendekeza uchoyo na ubinafsi usiokuwa na tija.

    Acha nihitimishe kwa kusema hivi Mavugo na Ajib wanapaswa kuonyesha ukomavu kwa kucheza kwa ajili ya timu na si mafanikio binafsi.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KWA HILI LA MAVUGO NA AJIB,OMOG UKO SAHIHI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top