728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, August 21, 2016

    OLIMPIKI;BRAZIL YAMALIZA GUNDU LA MIAKA MINGI,YASHINDA DHAHABU KATIKA SOKA LA WANAUME


    Rio de Janeiro,Brazil.

    BRAZIL imekata kitu ya kusubiri miaka nenda rudi kutwaa medali ya dhahabu baada ya Jumamosi Usiku kutwaa ubingwa wake wa kwanza wa michuano ya Olimpiki kwa upande wa soka la wanaume baada ya kuifunga Ujerumani kwa penati 5-4 kufuatia sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 120.

    Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Filho Maracana,Brazil ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao baada ya Neymar Jr kufunga dakika ya 25 ya mchezo kwa mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja langoni mwa Ujerumani.

    Ujerumani ilikuja juu na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha baada ya kiungo wake Max Meyer kufunga dakika ya 59 ya kipindi cha pili na kufanya mchezo kuisha kwa sare ya bao moja kwa moja.

    Katika dakika 30 za nyongeza hakuna timu iliyoweza kupata bao na ndipo hapo mikwaju ya penati ilipoamuliwa kutumika na wenyeji kuibuka washindi kwa penati 5-4 baada ya penati ya Nils Petersen kuchezwa na kipa wa Brazil,Weverton.

    Ubingwa huo ni wa kwanza kwa Wabrazil kuutwaa katika historia kwa michuano hiyo baada ya kupoteza fainali tatu hapo kabla.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: OLIMPIKI;BRAZIL YAMALIZA GUNDU LA MIAKA MINGI,YASHINDA DHAHABU KATIKA SOKA LA WANAUME Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top