728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, August 21, 2016

    DONE DEAL:JOEL CAMPBELL AIHAMA ARSENAL


    Lisbon,Ureno.

    SHAMBULIAJI wa kimataifa wa Costa Rica,Joel Campbell,ameihama Arsenal na kujiunga na Sporting Lisbon ya Ureno kwa mkataba wa mkopo wa msimu mmoja.

    Campbell,24,amejiunga na Sporting Lisbon baada ya kushindwa kuhakikishiwa namba katika kikosi cha kwanza cha Arsenal licha ya kufanya vizuri katika michezo ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu.

    Hii ni mara ya tano sasa kwa Campbell kuihama Arsenal kwa mkopo tangu alipojiunga nayo mwaka 2011 akitokea Derportiva Saprisa ya nyumbani kwao Costa Rica.

    Campbell anaiacha Arsenal kwa mara nyingine akiwa ameichezea jumla ya michezo 40 na kuifungia mabao manne katika michuano yote.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: DONE DEAL:JOEL CAMPBELL AIHAMA ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top