London,Uingereza.
Klabu ya Middlesbrough iliiyopanda ligi kuu ya England msimu huu imefikia makubaliano na klabu ya Arsenal kwa ajili ya kumsajili beki wake Calum Chambers kwa mkopo wa msimu mmoja.
Habari iliyochapishwa na tovuti rasmi ya Arsenal (Arsenal. Com) imesema miamba hiyo ya Emirates imeamua kutoa Chambers kwa mkopo kwa ajili ya kupata nafasi ya kucheza na kumuongezea uzoefu huku ikisisitiza kuwa klabu hiyo bado ina mipango mizuri na ya muda mrefu na beki huyo licha ya kuwa mbioni kutangaza usajili wa beki wa Valencia,Shkodran Mustafi.
Chambers mwenye umri wa miaka 21 sasa alijiunga na Arsenal mwaka 2014 akitokea Southampton kwa dau la £16m.
0 comments:
Post a Comment