Na.Chikoti Cico
Watford vs. Arsenal- Saa 11 jioni (Vicarage Road)
Ligi ya primia itaendelea kushika kasi wikendi hii ambapo Watford watawaalika Arsenal kwenye uwanja wao wa nyumbani, huku kila timu ikihitaji alama tatu baada ya Watford kupoteza mchezo uliopita na Arsenal kulazimishwa sare tasa.
TAARIFA ZA TIMU:
WATFORD.
Walter Mazzarri kocha wa Watford anatarajiwa kutokukibadilisha kikosi chake kilichocheza mchezo uliopita dhidi ya Chelsea na kufungwa kwa magoli 2-1. Wachezaji wapya waliosajiliwa klabuni hapo Daryl Janmaat, Younes Kaboul na Roberto Pereyra bado haijathibitika kama wataweza kuanza kwenye mchezo huo..
ARSENAL
Kiungo mahiri wa Arsenal Mesut Ozil anatarajiwa kuanza kwenye mchezo huo dhidi ya Watford baada ya kutokea benchi kwenye mchezo uliopita dhidi ya Leicester City wakati huo huo mshambuliaji wa klabu hiyo Olivier Giroud hatarajiwi kucheza mchezo huo.
Bado kocha wa Arsenal Wenger ataendelea kuwakosa Aaron Ramsey, Alex Iwobi, Per Mertesacker, Danny Welbeck na Carl Jenkinson ambao wote ni majeruhi.
TAKWIMU KUELEKEA MCHEZO HUO:
Watford wamepoteza michezo yote sita waliyocheza dhidi ya Arsenal ndani ya ligi ya primia ingawa waliwafunga Arsenal kwenye mchezo wa robo fainali ya kombe la FA kwa magoli 2-1 msimu uliopita.
Arsenal wameshinda michezo saba kati ya michezo nane waliyocheza dhidi ya Watford katika mashindano mbalimbali huku wakipoteza mchezo mmoja pekee,
Mara ya mwisho Watford kuifunga Arsenal kwenye mashindano ya ligi ilikuwa ni Aprili 1998, walishinda kwa goli 1-0 lililofungwa na Rick Holden.
Alexis Sanchez amehusika katika magoli matatu (magoli mawili na “assist” moja) dhidi ya Watford walipokutana katika michezo miwili iliyopita ya ligi ya primia.
Kiungo wa Watford Étienne Capoue amefunga katika michezo yote miwili ya klab hiyo kwenye msimu huu wa ligi, hakuna mchezaji wa Watford aliyewahi kufunga katika kila mchezo katika michezo mitatu ya ufunguzi wa ligi kuu.
Ni vikosi viwili pekee kwenye ligi ya primia vilivyokuwa na wastani wa umri wa miaka 30 na zaidi. Vyote ni vikosi vya Watford, wastani wa miaka 30 na siku 5 vs Southampton na wastani wa miaka 30 na siku 12 vs Chelsea.
VIKOSI VINAWEZA KUWA HIVI:
Watford XI:Gomes; Kaboul, Britos, Prodl, Janmaat; Behrami, Capoue, Pereyra, Zuniga; Deeney, Ighalo
Arsenal XI: Cech; Bellerin, Holding, Koscielny, Monreal; Xhaka, Coquelin; Oxlade-Chamberlain, Ozil, Sanchez; Giroud
0 comments:
Post a Comment