Al Ahli,Falme za Kiarabu.
MSHAMBULIAJI wa Kimataifa na Nahodha wa Ghana,Asamoah Gyan,amejiunga na klabu ya Al Ahli ya Falme za Kiarabu kwa mkopo wa msimu mmoja akitokea klabu ya Shanghai SIPG ya China na kukabidhiwa jezi namba 90.
Gyan,30,ambaye Jana Jumanne alitangazwa kufeli vipimo katika klabu ya Reading ya Uingereza amejiunga na Al Ahli leo jioni baada ya kufaulu vipimo vya afya alivyovifanya usiku wa kuamkia leo Jumatano.
Al Ahli imemsajili Gyan ili kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa Kimataifa wa Senegal,Moussa Sow,aliyerejea katika klabu yake ya zamani ya Fenerbahce ya Uturuki.
Hii ni mara ya pili kwa Gyan kujiunga na vilabu vya Falme za Kiarabu.Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2011 pale alipojiunga na Al Ain akitokea Sunderland.
Akiwa na Al Ain,Gyan,alifanikiwa kuifungia klabu hiyo mabao 128 katika michezo 123.Aliiwezesha Al Ain kutwaa mataji matatu huku yeye akiibuka mfungaji bora wa ligi mara tatu.
0 comments:
Post a Comment