728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, August 29, 2016

    MTANANGE WA YANGA,JKT RUVU ULIOKUWA UCHEZWE JUMATANO UMEAHIRISHWA


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    MTANANGE wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Mabingwa watetezi Yanga SC na Maafande wa JKT Ruvu uliokuwa ufanyike Jumatano ya wiki hii katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam umeahirishwa.

    Taarifa kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),zimesema mchezo huo uliopangwa kuchezwa Jumatano ya Agosti 31 ya mwaka huu sasa utachezwa tarehe nyingine ambayo bado haijaamuliwa.

    Hatua hiyo baada ya Yanga kuomba uahirishwe kwa sababu ina wachezaji wengi katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania,Taifa Stars.

    Wachezaji hao ni Deogratius Munishi 'Dida',Vincent Andrew 'Dante',Kelvin Yondani na Mwinyi Hajji, kiungo Juma Mahadhi na Simon Msuva.

    Wakati huohuo Yanga pia imesema wachezaji wake wengine,Vincent Bossou (Togo), kiungo Haruna Niyonzima (Rwanda) na mshambuliaji Amissi Tambwe (Burundi) nao pia wameitwa na timu zao za taifa na kufanya idadi ya wachezaji kufikia wanane.

    Kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara zinaruhusu timu ambayo wachezaji wake wasiopungua watano wameitwa timu za taifa kuahrishiwa mechi.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MTANANGE WA YANGA,JKT RUVU ULIOKUWA UCHEZWE JUMATANO UMEAHIRISHWA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top