London, Uingereza.
ARSENAL imeimarisha safu yake ya ulinzi kwa kumsajili mlinzi wa Ujerumani,Shkodran Mustafi,kutoka Valencia kwa ada ya £35millioni.
Mustafi,24,amesaini mkataba wa miaka mitano wa kuitumikia Arsenal baada ya kufaulu vipimo vyake vya afya alivyovifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Arsenal imeamua kumsajili Mustafi baada ya safu yake ya ulinzi kuwapoteza Per Mertesacker na Gabriel Paulista kwa majeruhi katika michezo ya kujiandaa na msimu mpya.
Mustafi alijiunga na Valencia mwaka 2014 akitokea Sampdoria kwa ada ya £6millioni.Kabla ya hapo aliwahi kupita katika klabu ya Everton lakini hakuwahi kuichezea mchezo wowote wa ligi kuu.
0 comments:
Post a Comment