Reading, England.
WAKATI heka heka za usajili zikikoleza kasi sehemu mbalimbali duniani, matukio ya wachezaji kufeli vipimo vya afya nayo yameendelea kutimua mbio kwa kasi ya ajabu na yenye kukatisha tamaa.
Ndoto ya Mshambuliaji wa Ghana,kujiunga na Reading kwa mkopo imebuma baada ya nyota huyo mwenye mbwembwe nyingi uwanjani kufeli vipimo vyake vya afya katika klabu hiyo inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini England.
Taarifa kutoka katika tovuti ya Reading imesema Gyan mwenye miaka 30 sasa amebainikiwa kuwa hayuko fiti kuichezea klabu hiyo kwa sasa na atahitaji zaidi ya wiki nane kurejea katika hali yake ya kawaida hivyo klabu imesitisha rasmi mpango wa kumsajili.
Hii ina maana kwamba Gyan aliyewahi kutamba na vilabu vya Rennes,Sunderland na Al Ain ya Abu Dhabi anarejea katika klabu yake ya Shanghai SIPG inayoshiriki ligi kuu ya nchini China.
Gyan anakuwa mchezaji wa pili kutoka Afrika kufeli vipimo katika kipindi kisichozidi masaa 72 baada ya Cheick Tiote kufeli vipimo vyake juzi usiku wakati akijiandaa kuijiunga na Galatasaray.
0 comments:
Post a Comment