Brussels, Ubelgiji.
KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Ubelgiji,Mhispania Roberto Martinez,amemteua nyota wa zamani wa Arsenal Mfaransa Thierry Henry kuwa msaidizi wake.
Martinez ametangaza uteuzi huo mchana wa leo wakati akitangaza kwa mara ya kwanza kikosi cha Ubelgiji ambacho mwezi Septemba kitacheza michezo miwili ya kimataifa dhidi Hispania Septemba 1 na Cyprus Septemba 6.
Mbali ya Henry,Graeme Jones,ambaye aliwahi kuhudumu kama msaidizi wa Martinez katika vilabu vya Wigan na Everton naye amejumuishwa katika benchi jipya la ufundi la Ubelgiji.Richard Evans amepewa ukufunzi wa viungo.
Martinez alipewa jukumu la kuifundisha Ubelgiji mwezi Julai mwaka huu baada ya aliyekuwa Kocha mkuu wa timu Marc Wilmots kubwaga manyanga baada ya timu hiyo kutolewa mapema katika fainali za Euro 2016.
Baadhi ya wachezaji ambao Martinez amewaita kuitumikia Ubelgiji ni Thiabaut Courtois,Toby Alderweireld, Jan Vertonghen, Kevin de Bruyne, Mousa Dembele, Marouane Fellaini,Michy Batshuayi, Eden Hazard, Romelu Lukaku, Kevin Mirallas na Divock Origi
0 comments:
Post a Comment