Genk,Ubelgiji.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania,Mbwana Ally Samatta,amefunga mabao mawili na kuiwezesha klabu yake ya KRC Genk kupata ushindi wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Lokeren katika mchezo safi wa ligi kuu Ubelgiji uliochezwa huko Diknam Stadion,Lokeren.
Samatta amepachika mabao hayo dakika za 34 na 38 akitumia vyema pasi murua za Alejandro Pozuelo kabla ya kutolewa dakika ya 73 na nafasi yake kuchukuliwa na Nikos Karelis.
Bao la tatu la KRC Genk limefungwa na Leon Bailey dakika ya 46 ya kipindi cha pili.Ushindi huo umeipeleka KRC Genk mpaka nafasi ya nne baada ya kufikisha alama saba kufuatia kushuka dimbani mara nne.
0 comments:
Post a Comment