London,Uingereza.
KOCHA wa Arsenal,Arsene Wenger,ameonyesha nia ya kutaka kuwauzia Real Madrid nyota wake raia wa Chile,Alexis Sanchez,katika kipindi hiki cha usajili ama kile cha mwezi Januari lakini kwa sharti la yeye kupewa wachezaji wawili.
Kwa mujibu wa gazeti la Don Balon ni kwamba wachezaji wanaotakiwa na kocha Arsene Wenger ni Mcolombia James Rodriguez pamoja na Mhispania Alvaro Morata.
Alvaro Morata
Don Balon limeendelea kupasha kuwa Arsenal imesema kuwa katika dili lolote lile la kumtaka Sanchez lazima Real Madrid imjumuishe mshambuliaji wake Alvaro Morata,vinginevyo hakutafanyika biashara ya aina yoyote ile.
Wakati huohuo taarifa kutoka nchini Italia zinasema Inter Milan nayo imejitosa kumwania Sanchez na tayari imeshaandaa ofa ya €80m ili kuhakikisha inamsajili katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya.
0 comments:
Post a Comment