Alexandria,Misri.
STRAIKA wa Cameroon,Samuel Nlend,amevunjiwa mkataba na klabu yake mpya ya Al Ittihad ya Misri baada ya kugundulika kuwa ana maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Nlend,21,ambaye siku nne zilizopita aliingia kandarasi ya miaka mitatu ya kuitumikia klabu hiyo yenye maskani yake katika jiji la Alexandria akitokea klabu ya Union Douala ya nyumbani kwao Cameroon amevunjiwa mkataba wake leo Jumatatu.
Taarifa za kuvunjwa kwa mkataba wa straika huyo aliyeichezea timu ya taifa ya Cameroon michezo minne na kuifungia bao moja imetolewa kwa vyombo vya habari vya Misri na msemaji wa Al Ittihad mchana wa leo.
Hatua hiyo ya Al Ittihad kumvunjia mkataba Nlend imekosolewa vibaya na watetezi wa haki za binadamu ulimwenguni na kuitwa kuwa ni ya kinyama.
0 comments:
Post a Comment