London,Uingereza.
Chelsea imetangaza kufanikiwa kumsajili mlinzi wa kushoto wa Hispania,Marcos Alonso Mendoza, kutoka Fiorentina kwa ada ya £20m.
Taarifa iliyochapishwa katika mtandao wa Fiorentenia imesema Alonso,25, mwenye uwezo wa kucheza pia beki ya kati ameihama klabu hiyo moja kwa moja na kujiunga na Chelsea kwa mkataba wa miaka mitano.
Kabla ya kutua Fiorentina,Alonso,aliwahi kuvichezea vilabu vya Real Madrid,Bolton na Sunderland.Chelsea imeamua kumsajili Alonso ili kuiongezea nguvu safu yake ya ulinzi hasa upande wa kushoto ambao umekuwa ukimtegemea Cesar Azpilicueta peke yake.
Wakati huohuo klabu ya Werder Bremen ya Ujerumani imetangaza kumsajili winga Serge Gnabry kutoka Arsenal.
Gnabry,21,alijiunga na Akademi ya Arsenal akitokea Stuttgart,mpaka anaondoka Arsenal amefanikiwa kucheza michezo 11 ya ligi kuu.
0 comments:
Post a Comment