728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, August 23, 2016

    MO BEJAIA YAICHAPA MEDEAMA FC NA KUIFUATA TP MAZEMBE NUSU FAINALI SHIRIKISHO


    Bejaia,Algeria.

    MO BEJAIA imeungana na TP Mazembe kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la shirikisho Afrika baada ya jioni hii kuifunga Medeama FC ya Ghana kwa jumla ya bao 1-0 katika mchezo mkali wa mwisho wa kundi A wa hatua ya robo fainali/nane bora uliochezwa katika uwanja wa Stade de l'Unité Maghrébine ulioko mjini Beajaia,Algeria.

    Bao pekee la mchezo huo uliokuwa na vuta nikuvute nyingi limefungwa dakika ya 51 na Morgan Betorangal baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Medeama FC.

    Kwa matokeo hayo Mo Bejaia imefuzu nusu fainali baada ya kufikisha pointi nane sawa na Medeama FC lakini imefanikiwa kupenya kwa sheria ya head to head (kufungana).

    Katika mchezo wa awali uliochezwa huko Ghana mwezi mmoja uliopita timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana hivyo bao moja la mchezo wa leo limeipa haki Mo Bejaia kusonga mbele licha ya kulingana pointi na Medeama FC.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MO BEJAIA YAICHAPA MEDEAMA FC NA KUIFUATA TP MAZEMBE NUSU FAINALI SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top