728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, August 22, 2016

    SAKATA LA HASSAN KESSY LABISHA HODI FIFA



    Dar Es Salaam,Tanzania.

    SIMBA wanatarajia kubisha hodi Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA), baada ya Kamati ya Sheria, Hadhi ya Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kumuidhinisha beki wao wa zamani, Hassan Ramadhani ‘Kessy’ kuichezea Yanga katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

    Uamuzi wa Simba kwenda FIFA unatokana na malalamiko yao yaliyowasilishwa kwa kamati hiyo dhidi ya Yanga kutupwa, huku Kessy akiidhinishwa Yanga.

    Simba waliwasilisha malalamiko kwa TFF wakidai Kessy kuwalipa Dola 60,000, sawa na Sh milioni 126 kutokana na kuvunja mkataba uliokuwa umalizike Juni 15, mwaka huu.

    Akizungumza jana, kiongozi wa juu wa Simba, ambaye hakutaja jina lake lifahamike,alisema wanatarajia kutinga FIFA, baada ya kutoridhika na uamuzi wa Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji TFF.

    Kiongozi huyo alisema kamati ya utendaji ya klabu hiyo ilitarajia kukutana jana jioni kwa ajili ya kujadili pamoja na mambo mengine,uamuzi huo wa TFF kabla ya kulipeleka FIFA.

    Alisema uamuzi wa kutafuta haki katika chombo kingine cha juu unatokana na malalamiko yao mengi yanayowasilishwa TFF kupuuzwa.

    Katika hatua nyingine, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, alisema baada ya kikao cha kamati ya utendaji jana,anatarajia kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu sakata la Kessy.

    Kessy alishindwa kuichezea Yanga kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika,baada ya Simba kuweka pingamizi kwa madai alikuwa hajamaliza mkataba.

    Lakini kamati ya Sheria, Hadhi na Wachezaji ya TFF, wiki iliyopita ilimuidhinisha kuichezea Yanga, huku ikiwataka Simba kumalizana na Kessy.

    Wakati huo huo, beki wa timu hiyo, Janavier Bokungu na kiungo, Mussa Ndusha, bado wataendelea kutoitumikia timu hiyo kutokana na uhamisho wao kimataifa (ITC) kuchelewa.

    Katibu wa Simba, Patrick Kahemela, alisema wanaendelea kushughulikia uhamisho wao ili waweze kuitumikia timu hiyo.

    “Tuliomba ITC kutoka Darling Club (DC Motema Pembe), lakini hazijafika,tunaendelea kufuatilia na mchezo ujao wanaweza,” alisema.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SAKATA LA HASSAN KESSY LABISHA HODI FIFA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top