728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, August 27, 2016

    UCHAMBUZI:CHELSEA VS BURNLEY- SAA 11 JIONI (STAMFORD BRIDGE)


    Na.Chikoti Cico.

    Ligi kuu nchini Uingereza itendelea wikendi hii ambapo katika uwanja wa Stamford Bridge wenyeji klabu ya Chelsea watawakaribisha Burnley. Klabu zote hizi mbili zina alama sita kwenye msimamo wa ligi ya primia.

    TAARIFA ZA TIMU:

    CHELSEA.

    Kuelekea mchezo huo kiungo wa Chelsea Willian anaweza kurejea uwanjani baada ya kukosa mchezo uliopita dhidi ya Watford kwa kuwa majeruhi ila itategemea na vipimo vya mwisho kuthibitisha kama atakuwa fiti kuwakabili Burnley.

    BURNLEY

    Kocha wa Burnley Sean Dyche kwenye mchezo huo dhidi ya Chelsea anatarajiwa kukichezesha kikosi kilichoshinda magoli 2-0 dhidi ya Liverpool hapo wikendi iliyopita.

    TAKWIMU KUELEKEA MCHEZO HUO.

    Chelsea haijafungwa mchezo wowote kati ya michezo minne iliyocheza na Burnley kwenye ligi ya primia huku ikishinda michezo mitatu na kutoka sare mchezo mmoja.

    Burnley imeweza kupata angalau goli moja ama zaidi katika michezo yote nane iliyocheza na Chelsea katika mashindano mbalimbali kasoro mchezo mmoja tu waliofungwa magoli 3-0 hapo Agasti 2009.

    Beki wa Chelsea Branislav Ivanovic alifunga katika michezo yote miwili ya msimu wa 2014/15 aliyocheza dhidi ya Burnley.

    Mara mbili Chelsea walipochukua ubingwa wa ligi ya primia klabu ya Burnley ilikuwa ipo daraja la kwanza.

    Burnley wamefungwa goli moja tu katika michezo yake mitano iliyopita ya ligi ya primia (mitatu ikiwa ni mwezi Mei 2015 na mingine miwili ni mwezi Agasti 2016)

    Klabu ya Chelsea imefungwa mchezo mmoja tu iliyocheza kati ya michezo 45 iliyopita ya ligi ya primia waliyocheza nyumbani dhidi ya klabu iliyopanda daraja. Walifungwa msimu uliopita na Bournemouth kwa goli 1-0.

    Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa amefunga magoli saba kati ya michezo tisa ya ligi ya primia aliyocheza mwezi Agasti.

    Burnley wamepata alama mbili tu kati ya michezo 11 iliyopita ya ligi ya primia waliyocheza jijini London, huku wakitoka sare michezo miwili na kufungwa michezo tisa na kufunga magoli sita huku wakichapwa magoli 28.

    VIKOSI VINAWEZA KUWA HIVI:

    Chelsea XI: Courtois; Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta; Matic, Kante; Hazard, Fabregas, Willian; Diego Costa

    Burnley XI: Heaton; Flanagan, Keane, Mee, Ward; Boyd, Marney, Defour; Arfield; Gray, Vokes



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: UCHAMBUZI:CHELSEA VS BURNLEY- SAA 11 JIONI (STAMFORD BRIDGE) Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top