728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, August 28, 2016

    VPL:YANGA SC YAUANZA MSIMU MPYA KWA TABASAMU YAICHAPA AFRICAN LYON 3-0 U/TAIFA


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    YANGA SC imeuanza vyema na kwa tabasamu pana msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya jioni ya leo kuchomoza na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya African Lyon katika mchezo safi uliochezwa katika uwanja wa taifa,Dar Es Salaam.

    Yanga SC ambayo leo ilikuwa inacheza mchezo wake wa kwanza wa msimu mpya wa 2016-17 ikitokea katika michuano ya shirikisho Afrika ilijipatia bao lake la kwanza dakika ya 18 ya kipindi cha kwanza kupitia kwa kiungo wake Deus Kaseke.Kaseke alifunga bao hilo akimalizia Kazi nzuri ya Simon Msuva na kuifanya Yanga SC iende mapumziko ikiwa mbele kwa bao hilo moja.

    Kipindi cha pili Yanga SC iliongeza kasi na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 59 kupitia kwa Simon Msuva aliyeiwahi pasi ndefu ya Thabani Kamusoko na kumchambua kipa wa African Lyon aliyetoka langoni akijaribu kumzuia.

    Bao la tatu la Yanga SC limefungwa dakika ya 94 na Juma Mahadhi kwa shuti kali baada ya kumegewa pasi safi na Yussuf Mhilu aliyekuwa ameingia uwanjani kuchukua nafasi ya Deus Kaseke.


     


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: VPL:YANGA SC YAUANZA MSIMU MPYA KWA TABASAMU YAICHAPA AFRICAN LYON 3-0 U/TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top