Na.Chikoti Cico
Klabu ya Hull City inayofundishwa na kocha msaidizi wa zamani wa Manchester United Mike Phelan itaikaribisha Manchester United kwenye uwanja wao wa KCOM, timu zote mbili zina alama sita kwenye msimamo wa ligi ya primia.
TAARIFA ZA TIMU:
HULL CITY
Kuelekea mchezo huo beki wa katikati wa Hull, Harry Maguire anaweza kucheza mchezo wake wa kwanza chini ya kocha wa muda wa klabu hiyo Mike Phelan baada ya kuwa nje kwa muda mrefu akiwa majeruhi. Ingawa kocha huyo atamkosa Greg Luer kwa wiki kadhaa baada ya kupata majeraha ya goti.
MANCHESTER UNITED
Kocha wa Manchster United Jose Mourinho anatarajiwa kuwa na kikosi kamili kuelekea mchezo huo dhidi ya Hull ukiachana na Jesse Lingard ambaye amekosa michezo miwili iliyopita ya ligi kwasababu ya majeruhi ingawa amethibitisha kurejea mazoezini.
TAKWIMU KUELEKEA MCHEZO HUO:
Hull City wamepoteza michezo 10 na kutoka sare mchezo mmoja kati ya michezo 11 iliyopita waliyocheza dhidi ya Manchester United katika mashindano mbalimbali. Mara ya mwisho Hull kuifunga United ni Novemba 1974 kwa magoli 2-0.
Man Utd wameshinda michezo mitatu kati ya minne iliyopita ya ligi ya primia waliyocheza kwenye uwanja wa KCOM Stadium na kutoka sare mchezo mmoja ingawa kwenye miwili iliyopita mchezaji wa United aliyocheza kadi nyekundu.
Nahodha wa United Wayne Rooney kiujumla amehusika katika magoli 10 ya klabu hiyo katika michezo sita ya ligi aliyocheza dhidi ya Hull, amefunga magoli saba na kutoa pasi (assists) tatu za magoli.
Hull City imeshinda michezo yake miwili ya awali kwenye ligi ya primia msimu huu wa 2016/17, klabu iliyopanda daraja na kushinda michezo yake mitatu ya awali ya ligi ya primia ni Bolton Wanderers msimu wa 2001/02.
Katika michezo 49 kati ya michezo 58 ya ligi aliyopoteza Jose Mourinho kama meneja amepoteza akiwa ugenini ambayo ni sawa na asilimia 84%.
Kocha wa muda wa Hull City Mike Phelan alikuwa kocha msaidizi wa Manchester United kati ya Septemba 2008 na Mei 2013 ambapo United walinyakua vikombe vitatu vya ligi ya primia.
Kiungo wa Hull City Ahmed Elmohamady ni “mtumishi mwaminifu” wa klabu hiyo kwani amecheza kila mchezo katika michezo yote 78 ya ligi ya klabu hiyo tangu 2013/14.
VIKOSI VINAWEZA KUWA HIVI:
Hull City XI:Jakupovic; Elmohamady, Livermore, Davies, Robertson; Meyler, Huddlestone, Clucas; Snodgrass, Hernandez, Diomande
Manchester United XI: De Gea; Valencia, Smalling, Blind, Shaw; Pogba, Fellaini; Mkhitaryan, Rooney, Martial; Ibrahimovic
0 comments:
Post a Comment