Barcelona, Hispania.
Barcelona imeendelea na pilika pilika za kukiongezea nguvu kikosi chake ili kuhakikisha inatisha zaidi msimu huu hii ni baada ya muda mfupi uliopita kutangaza kukamilisha usajili wa Mshambuliaji, Paco Alcacer,kutoka Valencia kwa mkataba wa miaka mitano.
Alcacer mwenye umri wa miaka 23 amejiunga na Barcelona kwa ada ya awali ya €30m ambayo itaongezeka kwa €2m kutokana na malipo ya bonasi.
Alcacer ambaye msimu uliopita alifunga mabao 13 na kutengeneza mengine sita amewekewa kipengele cha kuihama Barcelona kwa ada ya €100m.
Akiongea baada ya kukamilisha usajili wake Barcelona,Alcacer,amesema "Nilipojua kuwa kuna ofa kutoka Barcelona kwa ajili yangu,niliuomba uongozi wa Valencia kuipokea kwani niliona ulikuwa ni muda wa kujiendeleza zaidi.Licha ya kwamba nimeihama Valencia lakini bado itaendelea kubaki moyoni kwangu.
Alcacer anakuwa mchezaji wa sita kujiunga na Barcelona katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya.Wengine ni Jasper Cillessen, Andre Gomes, Samuel Umtiti, Lucas Digne na Denis Suarez.
Wakati Alcacer akijiunga na Barcelona,Munir El-Haddadi ameihama klabu hiyo na kujiunga na Valencia kwa mkopo wa msimu mmoja wenye kipengele kwa kusajiliwa moja kwa moja mwishoni mwa msimu.
0 comments:
Post a Comment