728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, August 30, 2016

    JACK WILSHERE KUIHAMA ARSENAL NDANI YA MASAA MACHACHE YAJAYO


    London,Uingereza.

    JACK Wilshere ataihama Arsenal kwa mkopo katika kipindi kifupi kilichobaki kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili Jumatano ya wiki hii.

    Taarifa za kuaminika zinadai kuwa tayari Wilshere ameshapewa ruhusu kuihama Arsenal hii ni baada ya kufanya mazungumzo ya kina na kocha wa klabu hiyo,Mfaransa Arsene Wenger.

    Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku moja tu imepita tangu nyota huyo aachwe nje ya kikosi cha England na Kocha Mpya,Sam Allardyce,kwa madai kuwa amekuwa hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara katika klabu yake ya Arsenal.

    Wakati huohuo taarifa kutoka ndani ya klabu ya Arsenal zinasema licha ya nyota huyo kuruhusiwa kuondoka kwa mkopo lakini bado yupo kwenye mipango ya muda mrefu ya klabu hiyo yenye makazi yake katika dimba la Emirates.

    Msimu huu Wilshere ameicheza Arsenal dakika 37 pekee,akishuka dimbani katika mchezo dhidi ya Leicester City na Watford na yote akitokea benchi.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: JACK WILSHERE KUIHAMA ARSENAL NDANI YA MASAA MACHACHE YAJAYO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top