Buenois Aires,Argentina.
BAADA ya kufanikiwa kumshawishi na kumrejesha kikosini Staa wa Barcelona,Lionel Messi,Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Argentina,Edgardo Bauza,ametangaza kikosi cha wachezaji 27 kitakachocheza michezo miwili ya kusaka tiketi ya kufuzu michuano ya kombe la dunia la mwaka 2018 dhidi ya Uruguay na Venezuela mwezi Septemba.
Aidha Katika kikosi hicho,Bauza,amemwacha Mshambuliaji Mpya wa Juventus,Gonzalo Higuain,huku akiwaita kwa mara ya kwanza nyota wa River Plate,Lucas Alario na Lucas Pratto wa Atletico Mineiro.
Septemba 6 mwaka huu Argentina,itashuka dimbani huko Mendoza kuvaana na wageni wao Uruguay kabla ya siku tano baadae yaani Septemba 11 kusafiri mpaka Merida kucheza na Venezuela.
Kikosi Kamili
Makipa: Sergio Romero (Manchester United),Mariano Andujar (Estudiantes),Nahuel Guzman (Tigres).
Mabeki: Facundo Roncaglia (Celta),Mateo Musacchio (Villarreal), Ramiro Funes Mori (Everton),Emmanuel Mas (San Lorenzo), Marcos Rojo (Manchester United), Martin Demichelis (Espanyol),Pablo Zabaleta (Manchester City), Gabriel Mercado (Sevilla), Nicolás Otamendi (Manchester City).
Viungo:Matias Kranevitter (Sevilla),Javier Mascherano (Barcelona), Lucas Biglia (Lazio), Augusto Fernandez (Atlético Madrid), Ever Banega (Inter), Javier Pastore (PSG), Erik Lamela (Tottenham),Nicolas Gaitan (Atletico Madrid), Angel Di MarÃa (PSG).
Washambuliaji:Lionel Messi (Barcelona), Angel Correa (Atletico Madrid), Lucas Pratto (Atletico Mineiro), Sergio Aguero (Manchester City), Paulo Dybala (Juventus), Lucas Alario (River).
0 comments:
Post a Comment