Hull,England.
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu England, Leceister City,wameuza vibaya msimu mpya wa ligi hiyo baada ya mchana wa leo kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Hull City katika mchezo mkali uliochezwa katika dimba la KC Stadium.
Mabao yaliyoipa Hull City ushindi huo muhimu yamefungwa na Adama Diomande dakika ya 46 na Robert Snodgrass dakika ya 57 kwa mkwaju mkali wa mbali huku lile la Leceister City likifungwa na Riyad Mahrez dakika ya 47 kwa mkwaju wa penati.
0 comments:
Post a Comment