Nairobi,Kenya.
Mshambuliaji wa Gor Mahia Michael Olunga [Injinia] jana usiku aliibuka kinara baada ya kutangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa ligi ya Kenya maarufu kama KPL.
Olunga ambaye siku chache zilizopita aliiwezesha Gor Mahia kutwaa ubingwa wa KPL amekuwa mchezaji wa nane kutwaa tuzo hiyo iliyoanza kutolewa mwaka 2008.
Mbali ya tuzo hiyo pia Olunga ameweka kibindoni kitita cha shilingi milioni 1.3 kama zawadi ya kuwa mchezaji bora na shilingi 300,000 baada ya kushika nafasi ya pili katika orodha ya wafungaji bora.
Nyota wengine waliong'aa usiku wa jana kwa kutwaa tuzo mbalimbali ni Boniface Oluoch wa Gor Mahia aliyetwaa tuzo ya kipa bora, Karim Nizigiyimana mlinzi bora,Eric Johana wa Mathare United akitwaa tuzo ya kiungo bora huku tuzo ya kocha bora ikienda kwa Frank Nuttall.
Nyota waliowahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka KPL miaka ya nyuma
2008 – Francis Ouma
2009 – John Baraza
2010 – George Odhiambo
2011 – Kevin Kimani
2012 – Danny Sserunkuma
2013 – Jacob Keli
2014 – Ekaliani Ndolo
0 comments:
Post a Comment