Kiungo wa Arsenal Mathieu Flamini huenda akajiunga na klabu ya Galatasaray ndani ya masaa 48 yajayo toka sasa.
Taarifa toka England zinasema Arsenal imekubaliana karibu kila kitu na Galatasaray kilichobaki ni mambo madogo tu kabla ya kiungo huyo mwenye miaka 31 hajamwaga wino wa kuichezea miamba hiyo ya Uturuki.
Ikiwa Flamini atakamilisha uhamisho huo atakuwa ni mchezaji wa pili wa Arsenal kutua Galatasaray baada ya Lukas Podolski.
0 comments:
Post a Comment