Klabu ya Azam imeanza vyema michuano ya kombe la Kagame baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya klabu ya KCCA ya Uganda katika mchezo mkali ulioisha hivi punde katika dimba la Uwanja wa Taifa,Dar es salaam.
Goli lililoipa ushindi Azam FC lilifungwa na mshambuliaji wake mahiri John Bocco dakika ya 12 ya mchezo akiunganisha pasi nzuri ya mlinzi Shomari Kapombe.
Katika mchezo wa mapema klabu ya Malakia ya Sudan kusini iliibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Adama City ya Ethiopia.
0 comments:
Post a Comment