Lollichon:Klabu ya Chelsea hatimaye imekubali kumruhusu kocha wake wa makipa Mfaransa Christophe Lollichon kuhamia klabu ya Arsenal.Lollichon amekuwa na mahusiano mabaya na kocha Jose Mourinho kwa kipindi kirefu sasa.Lollichon alitua Chelsea mwaka 2007 baada ya kupigiwa debe na kipa aliyehama klabuni hapo Peter Cech.
Isco:Klabu ya Juventus imepania kumsajili winga wa Real Madrid Isco na katika kutimiza dili hilo miamba hiyo ya Italia iko tayari kumjumuisha katika mpango huo mshambuliaji wake Fernando Llorente.( La Stampa)
Nasri:Klabu ya Juventus inataka kuibomoa klabu ya Manchester City kwa kumsajili kiungo wake Mfaransa Samir Nasri,29.( Tuttosport)
Moreno;Milinzi wa Liverpool Alberto Moreno na mlinzi wa Tottenham Jan Vertonghen ni kati ya majina mengi yanayowindwa na klabu ya Barcelona kuziba nafasi ya mlinzi wa klabu hiyo anayetaka kutimka klabuni hapo Adriano Correira.Wengine ni Wolfsburg Ricardo Rodriguez wa Wolfsburg na Layvin Kurzawa wa Monaco.( Mundo Deportivo)
Campbell:Klabu ya Palermo ya Italia inataka kumsajili kwa mkopo mshambuliaji kinda wa Arsenal Joel Campbell ili kumpa muda mwingi wa kucheza.Ikiwa Campbell atatua Palermo atakuwa ameeweka rekodi ya kuchezea vilabu vingi kwa mkopo katika kipindi cha muda mfupi.Campbell amecheza Ufaransa,Hispania (Mara mbili) na Ugiriki.(Gazzetta dello Sport)
Nolito:Klabu ya Barcelona imekanusha habari zinazodai kuwa inajipanga kumsajili winga wa Celta Nolito ili kuchukua nafasi ya Pedro.Wakati huohuo Barcelona imesisitiza kuwa bei ya kumuuza Pedro ( buyout clause) ni €150m (£106.2m) na siyo €30m (£21.2m).(Cadena Cope)
Belhanda:Klabu ya Lyon imetuma ofa kwenye katika klabu ya Dynamo Kiev kwa ajili ya kumsajili winga Younes Belhanda baada ya kupata habari mbaya kuwa nyota wake Clement Grenier hataweza kucheza tena msimu huu baada ya kuumia.(beIN SPORTS)
Telles:Klabu ya Chelsea imemuongeza katika orodha ya nyota inaowataka mlinzi wa kushoto wa Galatasaray Mbrazil Brazil Alex Telles ikiwa itashindwa kumsajili mlinzi wa Augsburg Abdul Baba Rahman ili kuziba nafasi iliyoachwa wazi na mlinzi Filipe Luis aliyerejea Atletico Madrid baada ya kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha kocha Jose Mourinho.
0 comments:
Post a Comment