San Francisco,Marekani.
Manchester United imeibuka na ushindi mnono wa goli 3-1 dhidi ya Barcelona katika mchezo mkali wa michuano ya International Champions Cup uliopigwa katika dimba la Levi's,San Fransisco,Marekani.
Ikicheza mbele ya mashabiki 68,000 Manchester United ilijipatia magoli yake kupitia kwa Wayne Rooney,Jesse Lingard na Adnan Januzaj huku lile la Barcelona likifungwa na kiungo Rafinha.
Katika mchezo mwingine Chelsea iliibuka na ushindi wa penati 6-5 dhidi ya PSG katika mchezo mwingine mkali uliopigwa huko Cherlotte,Marekani baada ya dakika tisini kuisha matokeo yakiwa sare ya goli 1-1. Zlatan Ibrahimovic aliifungia PSG goli kabla ya Chelsea kusawazisha kupitia kwa winga Victor Moses ambaye alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mtanange huo.
PENATI
Waliokosa:Juan Cuadrado (Chelsea) Jean-Christophe Bahebeck na Thiago Silva (PSG)
COURTOIS AFUNIKA
0 comments:
Post a Comment