HUENDA Simba ikawa inacheza mchezo wa pata potea kwa straika, Laudit Mavugo wa Vital’O baada ya klabu hiyo ya Burundi kuweka bayana kwamb
a kama Simba haitaweka mzigo mezani basi isitarajie kumpata.
Simba ilikurupuka na kwenda kufanya mazungumzo na
Mfungaji Bora huyo wa Ligi Kuu Burundi, kisha kusaini naye mkataba wa
miaka miwili na kumpa chake dola 10,000 (Sh20 milioni) kati ya dola
20,000 walizokubaliana.
Hata hivyo Rais wa Vital’O, Bikolimana Benjamin,
alisema klabu hiyo haipo tayari kumwachia Mavugo kama Simba haitatoa
dola 100,000 (Sh200 milioni) ili kuvunja mkataba wa mwaka mmoja uliobaki
baina yao na straika huyo.
Msimamo huo wa umeiweka Simba katika wakati mgumu
ambapo sasa taarifa za ujio wa mchezaji huyo ni za kupigwa kalenda kila
siku huku ikielezwa kwamba tayari tiketi ya kuja nchini ilitumwa kwa
straika huyo ambaye ameonyesha mapenzi dhahiri ya kutua Msimbazi.
Simba ilifanya mazungumzo na Mavugo na kukubaliana
katika kila kitu ambapo ingempatia dola 20,000 (Sh 40 milioni) kama ada
ya usajili na tayari walishatoa dola 10,000 (Sh 20 milioni) kama
kishika uchumba.
Benjamini aliliambia Mwanaspoti akisema:
“Tulifanya mazungumzo ya awali na Simba, lakini mpaka sasa bado
hawajatupa jibu kuhusiana na fedha hiyo, walituambia kwamba wangekuja
jana (juzi) au leo (jana) ila mpaka sasa hatujamwona kiongozi wao
yeyote.
“Tuliwaambia watulipe dola 100,000, wakilipa hizo
tutamwachia Mavugo ama timu yoyote ambayo itakuwa tayari kwa hilo maana
makubaliano waliyofanya na Mavugo sisi hatuyatambui.
“Linalotushangaza wamemalizana na mchezaji wakati bado ana mkataba na sisi.”
Taarifa za awali zilieleza kwamba Vital’O ilitaka
ipewe dola 60,000 (Sh 120 milioni) kama ada ya usajili ya straika huyo
lakini Simba ilikuwa tayari kutoa dola 30,000(Sh 60 milioni) ambazo sasa
wamezigomea na kupandisha hadi dola hizo 100,000.
Rais wa Simba, Evans Aveva
ambaye alikiri juu ya shinikizo hilo, lakini alidai fedha hizo za dola
100,000 ni nyingi mno kwao.
“Fedha hiyo ni nyingi mno na hatuna uwezo wa
kuitoa ila tunataka kuonana na kiongozi wa Shirikisho la Soka la Burundi
ambaye amekuja hapa ili tuone yeye atatusaidiaje juu ya hilo, barua yao
ya mwanzo hawakutaja kiasi hicho tunashangaa wamebadilika ghafla,”.
Kwa upande wa Mavugo ambaye anaonekana kuwa na kiu
ya kukipiga Msimbazi alisema: “Mimi nipo tayari kwa safari muda wowote
nitakapoambiwa mambo yao yamekamilika kati ya viongozi wa Simba na
Vital’O.
(mwanaspoti)
(mwanaspoti)
0 comments:
Post a Comment