Michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na kati maarufu kama kombe la Kagame inaendelea leo kwa mechi tatu kupigwa.
Mchezo wa kwanza unaopigwa uwanja wa Taifa unawakutanisha Khartoum ya Sudan dhidi ya KMKM ya Zanzibar saa 8 mchana, huku uwanja wa Karume saa 10 jioni KCCA ya Uganda wakiwakaribisha Adama City kutoka Ethiopia.
Katika uwanja wa Taifa majira ya saa 10 jioni, Telecom ya Djibout watakuwa wenyeji wa Yanga SC ambayo kocha wake mkuu Hans Van Der Pluijm ameahidi kupata ushindi katika mchezo huo.
Mechi ya ufunguzi, Yanga walifungwa 2-1 na Gor Mahia, hivyo ushindi ni muhimu katika mechi ya leo.
0 comments:
Post a Comment