728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, June 17, 2016

    MBAYA:KIUNGO QPR AFELI VIPIMO VYA AFYA URENO

    Lisbon,Ureno.

    NDOTO ya Queens Park Rangers kumpiga bei kiungo wake anayevuta mkwanja mrefu zaidi klabuni hapo, Mbrazil Sandro Raniere Guimarães Cordeiro maarufu kama Sandro imeyeyuka baada nyota huyo wa zamani wa Tottenham kufeli vipimo vyake vya afya katika klabu ya Sporting Lisbon ya Ureno.

    Sandro,27, ambaye tayari alikuwa amekubali kandarasi ya miaka mitatu ya kuichezea miamba hiyo ya Ureno huku Queens Park Rangers nayo ikikubali ada ya £1.5m kumwachia amejikuta akibaki njia panda baada ya vipimo kuonyesha kuwa goti lake moja lina matatizo.

    Tangu iliposhuka daraja kutoka ligi kuu mpaka ligi daraja la kwanza, Queens Park Rangers imekuwa ikihaha kuwaondoa mastaa wake wanaolipwa mishahara mikubwa.Tayari Queens Park Rangers imefanikiwa kuwaondoa Charlie Austin aliyetimkia Southampton na Rob Green aliyetemwa na sasa inahaha kumuondoa Sandro aliyelipwa £50,000 kwa wiki.

    Sandro alijiunga na QPR mwaka 2014 akitokea Tottenham Hotspur kwa ada ya £6m.Msimu uliopita alijiunga na West Bromwich Albion kwa mkopo wa miezi sita uliokuwa na kipengele cha kumnunua moja kwa moja kwa ada ya £4m lakini klabu hiyo ya Hawthorns iliamua kuachana na mpango huo baada ya kiungo huyo kuanza katika michezo mitano pekee ya Ligi Kuu England.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MBAYA:KIUNGO QPR AFELI VIPIMO VYA AFYA URENO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top