Manchester, England.
NI HESABU TU!!Manchester United imeamua kufanya kweli ili kuhakikisha kuwa inamnasa beki na nahodha wa Southampton,Mreno Jose Fonte,na kuwapiku wapinzani wao Arsenal ambao pia wanamtaka beki huyo mshindi wa Euro 2016.
Kwa nini Nasema Hesabu Tuu!!
Ishu iko hivi!!Manchester United ndiyo klabu ya kwanza kuonyesha nia ya kuitaka huduma ya Fonte mwenye miaka 32 sasa na tayari ilikuwa imeshaanza kujipanga kwa ajili ya kumsajili.
Sasa baada ya kusikia Arsenal nao wanamtaka beki huyo,Manchester United,wameamua kubadilisha gia na sasa wanataka kumtoa beki wao wa kushoto Marcos Rojo pamoja na pesa ili waweze kumpata Fonte kitu ambacho Arsenal hawawezi kukifanya.
Marcos Rojo
Wakati huohuo taarifa za ndani zinasema kuwa kocha wa Manchester United,Jose Mourinho,anataka kutumia uswahiba uliopo kati yake na Fonte ili kuizidi kete Arsenal kwani wote wawili wako chini ya wakala mmoja,Jorge Mendez.
0 comments:
Post a Comment