George James
Hatimaye klabu ya soka ya Chelsea leo imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa timu ya taifa ya Colombia Radamel Falcao,29 na kuka
bidhiwa jezi namba tisa (9).
Swali la kujiuliza ni kwamba, Je mshambuliaji huyo atarudi katika ubora wake wa zamani?Ni jambo la kusubiri nakuona kama The special One ataweza kumfanya arudi katika ubora wake mshambuliaji huyo aliyechemsha kwa mashetani wekundu wa Old trafford
Pili uwepo wa Cesc Fabregas pale darajani nao utamsaidia kuwika tena kutokana na pasi zake za mabao ni jambo la kusubiri nakuona
.Falcao anaungana na nyota wenzake wa zamani katika klabu ya Atletico Madrid ambao ni Thibaut Courtois, Filipe Luis na Diego Costa.
Wakati huo huo Chelsea imemtoa kwa mkopo kwenda Monaco kinda wake Mario Pasalic 20.
0 comments:
Post a Comment