Balotelli:Kocha wa Newcastle Steve McClaren amekana ripoti zinazosema kuwa klabu hiyo inafukuzua kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli.(Daily Star)
Manquillo:Baada ya kumsajili Nathaniel Clyne klabu Liverpool inapanga kuvunja mkataba wa mlinzi Javier Manquillo 21 aliyeko klabuni hapo kwa mkopo akitokea Atletico Madrid.(ESPN)
Wenger:Kocha Arsene Wenger anajiandaa kuwapiga bei nyota wake sita katika mkakati wa kukisuka upya kikosi chake.Nyota watakaopigwa bei ni David Ospina,Joel Campbell,Yaya Sanogo,Carl Jenkinson,Lukas Podolski na Mathieu Flamini.(The Sun)
Adekanye:Liverpool imeendelea kutumia vizuri pesa zake baada ya kufanikiwa kuinasa saini ya kinda mwenye kipaji kikubwa Bobby Adekanye toka Barcelona.Adekanye 16 ambaye kiuchezaji ni kama nyota wa Bayern Munich Arjen Robben ni moja kati ya makinda waliosababisha Barcelona ifungiwe na FIFA kufuatia klabu hiyo kufanya udanganyifu katika masuala ya usajili.
Ramos:Real Madrid inajipanga kumuongezea mshahara mlinzi wake Sergio Ramos mpaka £200,000 kwa wiki ili kumshawishi aachane na mpango wa kutaka kutimkia Manchester United.Ikiwa Ramos atakubali ofa hiyo atakuwa nyota anayelipwa vizuri nyuma ya Gareth Bale na Cristian Ronaldo.(The Sun)
McCarthy:Tottenham inajipanga kuijaribu Everton kwa kutaka kumsajili kiungo James McCarthy na katika kufanikisha usajili huo miamba hiyo ya London imepanga kuwatoa Aaron Lenon na Younes Kaboul.(Daily Mail)
Stoke City:Stoke City inataka ipewe kwa mkopo nyota mmoja kati ya Victor Moses,Patrick Bamford au Ruben Loftus - Cheek kabla ya kukubali kumuuza Chelsea mlinda mlango wake Mbosnia Asmir Begovic.(The Sun)
Coleman:Manchester United inapanga kumtumia kama chambo mlinzi wake Johnny Evans ili kuishawishi Everton ikubali kumuuza mlinzi wake wa kulia Seamus Coleman.(Mail Mirror)
Pjanic:Kocha wa Atletico Madrid Muargentina Diego Simeone anataka kumsajili kiungo wa Roma Miralem Pjanic ili kuchukua nafasi ya Arda Turan lakini tatizo kubwa ni dau la €45m analouzwanyota huyo wa Bosnia
.
.
Podolski:Galatasaray imefanikiwa kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Lukas Podolski kwa ada ya €4m.Podolski amesaini mkataba wa miaka mitatu baada ya kuambiwa hayumo katika mipango ya kocha Arsene Wenger.(Bild)
0 comments:
Post a Comment