Mshambulizi wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars aliyekuwa anakipiga El Merrikh Allan Wanga amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Azam FC mchana huu na kukamilisha idadi ya wachezaji saba wa kimataifa.
Nyota wengine wa kigeni waliopo Azam FC ni Jean Baptiste Mugiraneza ‘Migi’ kutoka APR ya Rwanda na Serge Wawa Pascal, Kipre Michael Balou, Kipre Tchetche wote wa Ivory Coast, Brian Majwega wa Uganda na Didier Kavumbangu wa Burundi, ambao wote walikuwepo tangu msimu uliopita.
0 comments:
Post a Comment