Hatua ya nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) inatarajiwa kuendelea kesho katika uwanja wa Taifa, huku kiingilio cha chini katika michezo hiyo kikiwa ni shilingi elfu tatu (3,000).
Viingilio vingine vya michezo hiyo ya kesho ni VIP A ni shilingi elfu kuni na tano (15,000) na VIP B & C, Shilingi elfu kumi (10,000) na sehemu nyingine ya uwanja iliyobakia ni shilingi elfu tatu (3,000) kwa viti vya rangi ya bluu, kijani na rangi ya chungwa.
Timu nne kutoka katika nchi nne wanachama wa michuano hiyo, Azam FC (Tanzania), Gor Mahia (Kenya), KCCA (Uganda) na Al Khartoum (Sudan) zimefuzu kwa hatua ya nusu fainali itayochezwa uwanja wa Taifa siku ya ijumaa.
Mchezo wa kwanza utakaonza saa 7:30 mchana utazikutanisha timu za Gor Mahia ya Kenya itakayocheza dhidi ya Khartoum ya Sudan, mchezo unaotarajiwa kuwa wa vuta nikuvute kufutia timu hizo kutoka sare katika mchezo wake wa awali hatua ya makundi.
Katika mchezo wa kwanza uliozikutanisha timu hizo, kocha wa Khartoum Kwesi Appiah na Frank Nuttal wa Gor Mahia walitoka sare ya bao 1- 1 ndani ya dakika 90, hali ambayo inapelekea kufaya mchezow wa kesho kuwa mgumu kwa kila timu kuhitaji nafasi ya kusonga mbele hatua ya fainali.
Gor Mahia mabingwa mara tano wa michuano hiyo, wataingia uwanjani kusaka ushindi ili kusonga hatua ya fainali ili waweza kutwaa ubingwa huo kwa mara ya sita, sawa na klabu ya Simba inayoongoza kwa kutwaa ubingwa huo.
Kocha Frank Nuttal atakua akiwategemea wachezaji wake nyota, Khalid Alucho, Kagere Meddie, Michael Olunga, Sibomana Abouba, Karim Nzigiyimana, Godfrey Walusimbi, Nahodha Musa Mohamed, na mlinda mlango Boniface Oluoch katika kusaka ushindi dhidi ya Khartoum.
Kwesi Appiah atashuka dimbani akiwategemea wachezaji wake nyota, Antony Akumu, Dominic Abdui, Samawal Meshani, Wagdi Wawd, Ouismaila Baba na nahodha Amin Ibrahim.
Vita kali itakua kwa washambulaji Michael Olunga wa Gor Mahia na Salaheldin Osman wote wenye mabao manne, wakiwania kuongeza bao katika mchezo huo wa kesho ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa kiatu cha dhahabu.
Nusu fainali ya pili itawakutanisha waoka mikate wa Azam FC dhidi ya Mamlaka ya jiji la Kampala (KCCA), mchezo utaokanza majira ya 9:45 kwa saa za Afrika na Kati katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mchezo huo pia unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kufutia timu hizo katika mchezo wa hatua ya makundi, Azam FC kuibuka na ushindi wa bao 1- 0, bao liliofungwa na nahodha wake John Bocco.
KCCA chini ya kocha wake Mike Mutebi watashuka dimbani kusaka ushindi katika mchezo huo, ikiwa ni kulipiza kisasi kwa mchezo wa kwanza na kupata ushindi utakaowavusha mpaka katika hatua ya fainali.
Kocha Mutebi atakuwa akiwategmea wachezaji wake nyota, Nahodha Tom Matiko, Opio Emmanuel, Joseph Ochaya, Hassan Waswa, Isaac Sserenkuma, Habib Kavuma na Muzamil Mutyaba.
Azam FC itashuka dimbani kutaka kuendeleza ubabe wake dhidi ya KCCA ya Uganda, na kuweza kukata tiketi ya kucheza fainali siku ya jumapili katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kocha wa Stewart Hall wa Azam atakua akijivunia safu yake ya ulinzi ambayo haijaruhusu bao tangu kuanza kwa michuano hiyo, huku safu yake ya ushambuliaji ikiwa imefunga mabao 8 katika michezo mine iliyocheza.
Hall atashuka dimbani akiwategema nyota wake Nahodha John Bocco, Pascal Wawa, Aggrey Morris, Himid Mao, Kipre Tchetche, Jean Baptist Mugiranenza, Frank Domayo na mlinda mlango Aishi Manula.
0 comments:
Post a Comment