Gor Mahia wana uhakika wa kutinga robo fainali ya michuano ya Kagame baada ya ushindi wao wa pili leo dhidi ya timu za Tanzania.
Jumamosi wakati wa ufunguzi, waliifunga Yanga mabao 2-1, leo wamerudi tena kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuitandika KMKM kwa mabao 3-1.
Wakati Gor Mahia walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Myarwanda Meddy Kagere, KMKM walisawazisha mfungaji akiwa Anthony Simon.
Bao hilo liliamsha matumaini lakini wakashindwa kuwa ngangari katika kipindi cha pili na kuwaruhusu Wakenya hao kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Hata hivyo, safu ya ulinzi ya KMKM ilishindwa kumdhibiti mshambuliaji hatari wa Gor Mahia, Michael Olunga kufanya vitu vyake.
Olunga alifunga bao la pili katika dakika ya 70, kabla ya kupiga la tatu katika dakika ya 82 na kuihakikishia Gor ushindi huo wa pili mfululizo dhidi ya timu za Tanzania.
0 comments:
Post a Comment