Kwenye wengi, hakukosi mengi! Kijana mmoja amekuwa kati ya karibia 600 waliojitokeza kuwania kuichezea timu ya Simba ya vijana chini ya miaka 20.
Lakini kivutio zaidi ni kwamba kijana huyo, tayari ana pete ya ndoa ikionyesha ameishaoa na kitambi kuliko hata makocha wawili wa Simba waliokuwa wanasimamia zoezi hilo.
Yusuf Macho ‘Musso’ na Nico Kiondo ndiyo walikuwa makocha wanaosimamia zoezi hilo Uwanja wa Mwenge Shooting jijini Dar es Salaam.
Kijana huyo alikuwa kati ya vijana wanaopambana kuhakikisha wanapata nafasi ya kuichezea Simba B.
Hata hivyo, muonekano wake alianza kuonyesha ni mnyonge na taratibu alikuwa akijitenga.
Vijana karibu 600 walijitokeza kuwania nafasi ya kuichezea Simba B na kwa mujibu wa makocha hao, wachezaji 60 ndiyo walikuwa wanatakiwa katika awamu ya kwanza.
0 comments:
Post a Comment