Washington, Marekani.
Chelsea imeendelea kuvinyanyasa vilabu vinavyotoka nnje ya England baada ya alfajiri ya kuamkia leo kuibuka na ushindi wa penati 4-2 dhidi ya Barcelona katika mchezo mkali wa International Champions Cup uliopigwa huko Washington,Marekani.
Mpaka dakika tisini za muda wa kawaida zinafikia tamati timu hizo zilikuwa sare ya goli 2-2.Magoli ya Barcelona yalifungwa na Louis Suarez (52) na Sandro Ramirez (66) huku yale ya Chelsea yakifungwa na Eden Hazard (10) na Garry Cahill (85).
0 comments:
Post a Comment