Amelia:Klabu ya Arsenal huenda ikafanya usajili wa kushitukiza kwa kumsajili mlinda mlango mkongwe wa Juventud Marco Amelia ili kuchukua nafasi ya Wojciech Szczesny ambaye kesho jumatatu atajiunga na klabu ya AS Roma kwa mkopo wa msimu mmoja.(Sky Italia)
Diaby:Kiungo Abou Daiby amekubali kujiunga na klabu ya Marseille ya Ufaransa akiwa kama mchezaji huru baada ya kutemwa na klabu ya Arsenal.(L'Equipe)
Aubameyang:Mshambuliaji wa klabu ya Borussia Dortmund Mgaboni Pierre-Emerick Aubameyang ametupilia mbali uvumi wote unaodai kuwa anataka kuihama klabu hiyo na badala yake amesisitiza kuwa bado ana furaha kuendelea kuitumikia miamba hiyo ya Bundesliga. him with a move away from the Bundesliga.(Welt am Sonntag)
Capel:Everton imeanza kumtupia jicho winga wa Sporting Lisbon Diego Capel ili kuchukua nafasi ya winga wake Mbelgiji Kevin Mirallas anayetaka kutimkia klabu ya West Ham kwa dau la £10m.(the Sunday Express)
Mbemba:Newcastle imeshinda mbio za kumsajili mlinzi wa Anderlecht Chancel Mbemba,22 baada ya vipimo vyake vya afya kuonyesha yuko safi kinachosubiriwa ni kibari cha kufanyia kazi nchini England ambapo shauri hilo litafanyika alhamisi ya wiki ijayo.
Welbeck:Klabu ya Besiktas imeachana na mpango wa kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Danny Welbeck na badala yake itamsajili mshambuliaji wa Fiorentina Mario Gomez,30 ili kuchukua nafasi ya mshambuliaji Demba Ba aliyetimkia klabu ya Shanghai.Gomez mapema wiki ijayo atasaini mkataba wa miaka miwili ya kuwatumikia wababe hao wa Uturuki.(Daily Star)
Inan:Klabu ya Leicester imemuweka kwenye orodha yake ya usajili kiungo na nahodha wa Galatasaray Selcuk Inan ili kuziba pengo la kiungo Esteban Cambiasso aliyegoma kuongeza mkataba mpya.(The Daily Star)
Guardiola;Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola amekubali kuwa kocha mpya wa Manchester City akichukua nafasi ya Manuel Pellegrini.Guardiola,44 ataanza kuifundisha Manchester City msimu ujao wa 2016/17.(BeIN Sports)
0 comments:
Post a Comment