728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, July 21, 2015

    SIMBA SC:OLUNGA NENDA TU HATUKUWEZI SISI

    SI kwamba wanaigiza ila kwanza wanaangalia mfuko wao ukoje, halafu wanaangalia nafasi ambazo kwao ni muhimu kufanya marekebisho ndipo wanasajili.

    Simba wameangalia kiasi kilichotajwa kuwa ukitaka kumng’oa straika wa Gor Mahia, Michael Olunga mwenye miaka 21 lazima uwe na Dolla 50,000 sawa na Sh 100 milioni, wenyewe wamesema kwasasa atasubiri sana kupata fedha hizo.

    Hilo ni moja, pia wameangalia kwa umakini nafasi yake hiyo wameona hakuna haja ya kumbembeleza ili ashuke ukizingatia ana mkataba wa miaka minne na Gor, wakatamka tena kuwa Laudit Mavugo wa Vital’O anawatosha.

    Rais wa Simba, Evance Aveva ameliambia Mwanaspoti kuwa Olunga ni mzuri ila kwasasa hatakuwa na nafasi ya usajili Simba kwa kuzingatia mipango yao ingawa alikiri kumpa nafasi kipa wa Gor, Boniface Oluoch.
    “Olunga mzuri lakini hawana tofauti na Mavugo, fedha yake pia ni kubwa mno ila kipa bado tunamwangalia,’’ alisema.

    Mbali na Oluoch mchezaji mwingine aliyezua mjadala katika usajili wa Simba baada ya mechi ya Yanga na Gor ya Kombe la Kagame ni kiungo mkabaji, Aucho Khalid ingawa naye ana mkataba wa miaka miwili.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SIMBA SC:OLUNGA NENDA TU HATUKUWEZI SISI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top