Hekaheka za usajili zimeendelea kupamba moto baada ya jioni hii vilabu vya Italia na England kuendelea kuboresha vikosi vyao kwa kusajili wachezaji wapya tayari kabisa kwa msimu ujao wa ligi na michuano mingine.
INTER MILAN
Jovetic:Klabu ya Inter Milan imefanikiwa kuinasa kwa mkopo wa miezi 18 saini ya mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Stevan Jovetic,25.Baada ya mkopo huo kuisha Inter Milan itamsajili nyota huyo wa Montenegro.
ASTON VILLA
Klabu ya Aston Villa imekamilisha usajili wa nyota wawili kwa mpigo jioni ya leo baada ya kumnasa kiungo Mfaransa Jordan Veretout (22) kutoka Nantes na mshambuliaji Mbenin Rudy Gestede (26) toka klabu ya Blackburn Rovers.Ada za uhamisho bado hazijawekwa wazi.
0 comments:
Post a Comment