Westham imeshindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani wa Upton Park baada ya kulazimishwa sare ya goli 2-2 na klabu ya Astra Giurgiu ya Romania katika michezo ya raundi ya sita ya michuano ya Europa ligi jana usiku.Magoli ya Westham
yalifungwa na Enner Valencia na Mauro Zarate huku magoli ya wageni yakifungwa na Fernando Boldrin pamoja na lile la kujifunga la mlinzi mpya wa Westham Angelo Ogbonna.Westham pia ilimpoteza mlinzi wake Collins aliyelimwa kati nyekundu kwa kuonyesha mchezo mbaya huku Enner Valencia akipata majeraha.
Katika mchezo mwingine Southampton imeibugiza magoli 3-0 klabu ya Vitesse.Magoli ya Southampton yamefungwa na Graziano Pelle,Dusan Tadic na Shane Long.
Matokeo mengine ya Europa ligi ni kama ifuatavyo.....
- Kairat Almaty 2 - 1 Aberdeen
- West Ham 2 - 2 Astra Giurgiu
- Southampton 3 - 0 Vitesse
- IF Elfsborg 2 - 1 Odd
- AIK 1 - 3 Atromitos Athens
- Apollon Limassol 1 - 1 FK Qabala
- CASHPOINT SCR Altach 2 - 1 Vitória Guimarães
- FK Krasnodar 2 - 0 Slovan Bratislava
- PAOK Salonika 1 - 0 Spartak Trnava
- SK Puntigamer Sturm Graz 2 - 3 Rubin Kazan
- Slovan Liberec 2 - 1 Hapoel Ironi Kiryat Shmona
- AZ Alkmaar 2 - 0 Istanbul Basaksehir
Mechi za marudiano ni tarehe 6 Agosti
0 comments:
Post a Comment