Mshambuliaji wa Yanga, raia wa Liberia, Kpah Sherman sasa maisha yamefikia kikomo Jangwani baada ya kuuzwa rasmi.
Katibu mkuu wa Yanga, Dr. Jonas Tiboroha amethibitisha kumuuza Sherman katika klabu ya Black Aces inayoshiriki ligi kuu soka nchini Afrika Kusini.
Hata hivyo, Tiboroha amesema dau walilomuuza straika huyo ni siri yao.
Sherman aliyeuzwa moja kwa moja ameondoka kwa ndege jana majira ya saa moja usiku kuelekea Bondeni kwa Madiba ambako anakwenda kuanza maisha mapya.
Nyota huyo aliyeshindwa kuwika Jangwani alisajiliwa wakati wa dirisha dogo mwezi Desemba mwaka jana
0 comments:
Post a Comment